Vyombo vya habari vyawezasongesha agenda 2030 na kukuza haki za binadamu ni muhimu - Faraja Kihongole
MP3•Episod hem
Manage episode 461278676 series 2027789
Innehåll tillhandahållet av UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations. Allt poddinnehåll inklusive avsnitt, grafik och podcastbeskrivningar laddas upp och tillhandahålls direkt av UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations eller deras podcastplattformspartner. Om du tror att någon använder ditt upphovsrättsskyddade verk utan din tillåtelse kan du följa processen som beskrivs här https://sv.player.fm/legal.
Kundi la waandishi wa habari 15 wanawake kutoka nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania mwaka jana wa 2024 walitumia siku tano jijini Geneva, Uswisi kushiriki programu ya kushirikisha waandishi wa habari ili wapate uelewa wa kazi za Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu. Ufadhili wao ulikuwa kupitia mashirika mawili ya kiraia, Universal Rights Group (URG) na Friedrich Naumann Foundation. Wakiwa Geneva, walipata fursa ya kuzungumza mabalozi wanaowakilisha nchi zao kwenye Baraza hilo, wataalamu wa haki za binadamu, mashirika ya kiraia na waandishi wa habari ambao kituo chao cha kazi ni Baraza la Haki za Binadamu.Miongoni mwao ni Faraja Kihongole kutoka Africa Media Group Tanzania Limited. Alihojiwa na Pascal Sim, Afisa wa Mawasiliano katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu jijini Geneva kuhusu masuala kadhaa ikiwemo alichojifunza na anachoondoka nacho. Matokeo ya mahojiano hayo ndio makala ya leo inayoletwa kwako na Assumpta Massoi.
…
continue reading
100 episoder